Harmonize amgusa Zamaradi, Naye ashusha shukrani zake

Nyota wa muziki wa Bongo Fleva kutoka kundi la WCB, Harmonize amesema anafarijika sana kuona watu mbalimbali wanampa moyo na ujasiri wa kuendelea kupambana katika kuupeleka muziki wake mbele.
Harmonize amesema hayo kufuatia moja ya wahamasishaji wakubwa kuhusu masuala ya kimaisha nchini Zamaradi Mketema kumpa pongezi kwa juhudi kubwa anazozifanya katika kazi zake, hali inayozidi kumuimarisha katika tasnia ya muziki hapa nchini na nje ya mipaka ya Tanzania.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, Zamaradi amesema miaka kadhaa nyuma aliwahi kumtabiria nyota huyo kuwa mwanamuziki mkubwa na kwamba kwa sasa tayari Harmonize amefika alipomtabiria.


“Miaka kadhaa nyuma niliwahi kukwambia YOU ARE THE NEXT BIG THING, nakiri kusema umefikia hapo tayari, kuna vitu vingi mno unavyo ambavyo nitaelezea siku nyingine lakini acha niseme leo kutoka moyoni mwangu YOU ARE MY STAR, na nina uhakika kuna wengine wengi pia wanaokutazama hivyo.”

“Leo hata ukiamua kufanya Show Classy ya MTU MMOJA TU ukaweka kiingilio LAKI MOJA na zaidi nakuhakikishia UTAJAZA NA KUTAPISHA UKUMBI sababu you have all it takes, Congrats on Konde Gang pia, inaonesha husahau ulipotoka, na Hongera kwa mafanikio yote uliyonayo, you are POWERFUL, collected na una Strategies za namna yako.”

Zamaradi amemalizia kwa kusema, “Humbleness is the KEY, hivyo Endelea kuwa Humble as Ulivyo, Only Sky is the Limit @harmonize_tz.”

Juzi Harmonize alitambulisha wimbo wake mpya wa Never Give Up ambao mapokezi yake yamekuwa makubwa sana.

Posti ya Harmonize hii hapa.

Posti ya Zamaradi

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *