Baada ya kimya kirefu, Sugu ametangaza muda rasmi wa kustaafu

Joseph Osmund Mbilinyi maarufu kama Mr Two, 2 proud au Sugu ni mkongwe katika muziki wa kizazi kipya nchini hususan Hip hop na pia ni mbunge wa Mbeya Mjini kwa vipindi viwili sasa.

Kwa jinsi ambavyo Sugu anavyoipenda Mbeya unaweza kusema ndipo sehemu ambayo alizaliwa au ndio asili yake lakini ukweli ni kwamba Sugu alizaliwa mkoani mtwara katika hospitali ya Ligula. Sugu asili yake ni Songea mkoani Ruvuma (inawezekana akawa Mngoni) tofauti na watu wengi wanavyodhani kwamba ni mnyakyusa. Sugu alihamia mbeya mwaka 1987 baada ya baba yake kuhamishiwa kikazi mkoani humo.

Miaka ya tisni ndipo Sugu alipoanza rasmi harakati zake za muziki wa Hip hop, ikielezwa sababu kubwa ni kutokana na kufariki kwa baba yake hivyo alianza harakati hizo kwa nia ya kuelimisha lakini pia kujipatia kipato.
Ni mkongwe kweli kweli, pengine ndiyo miongoni mwa waanzilishi wa harakati za muziki wa Hip hop hapa Bongo na amefanya makubwa ya kukumbukwa.

Licha ya kupitia changamoto nyingi katika harakati zake, muziki umempa faida kubwa ikiwa ni pamoja na kutambulika kwa mamilioni ya Watanzania, hali iliyosababisha kujiingiza kwa mara ya kwanza kwenye siasa mwaka 2010 na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa kishindo na kufanikiwa kuibuka tena mshindi mwaka 2015 kwa ushindi mkubwa zaidi ya mbunge yeyote nchini.

Hata hivyo shughuli za ubunge zimeonekana kumfanya apunguze sana majukumu ya kimuziki ambapo sasa ni rasmi ametangaza kukaribia kuachia kipaza sauti kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo umri.

Katika ukurasa wa wa Instagram, Sugu amesema anakiri African Hip hop imemtoa mbali na yeye pia kuutoa mbali kwenye ardhi hii ya Bongo lakini kuliko kukaa kimya bila kufanya muziki anaona sasa ni wakati wa kutangaza kustaafu na muda si mrefu ataweka kipaza sauti chini.

Amesema sababu kubwa ni umri kumtupa mkono pamoja na kukabiliwa na majukumu mengine ambayo yanahitaji sana muda wake na kuongeza kuwa kwa sababu anawathamini mashabiki wake hawezi kuwaacha hivi. Ameweka machaguo mawili atakaytumia kuwaaga am ani kwa utoa albamu au concert (tamasha).

Inawezekana Sugu akawa ndiye msanii wa kizazi kipya mwenye album nyingi. Mpaka sasa ametoa album takribani tisa. Album hizi ni kama “Ni Mimi” iliyotoka mwaka 1995, Ndani ya Bongo (1996), Niite Mr II (1998), Nje ya Bongo (1999), Millennium (2000), Muziki na Maisha (2001), Itikadi (2002), Sugu (2004), Coming of Age-Ujio Wa Umri (2006) na VETO iliyotoka mwaka 2009.

Soma alichoandika hapa-:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *