Mwenye hela mpishe! Akothee atoa Shilingi milioni 2.2 kwa ada ya chuo kikuu cha binti

Image result for akothee and daughters

Kama huna habari kwamba Madam Boss ana hela basi kaa kitako ujionee mwenyewe.

Mtoto wa tatu wa Akothee, Prudence Okello almaarufu Fancy Makadia hivi karibuni alijiunga na chuo kikuu cha kifahari nchini Ufaransa.

Related image

Akothee anatoa takriban shillingi milioni mbili nukta mbili kwa karo ya shule.

Kupitia kwa mtandao wa kijamii, Akothee aliandika;

Mtoto wangu anajiunga na chuo kikuu. Leo nimemchukua mtoto wangu akajiunge na shule ya ndoto zake. Ukiwa na mama yako ambaye ni wa kimataifa. Karo ya shule ni Euro 20,000 ikitegemea kosi.

Image result for akothee and daughters

Naam, bintiye Akothee mwenye umri wa miaka 19 alifanya viwango vyake vya O-levels katika shule ya kifahari ya Braeburn ya Mombasa, ambapo alijifunza na ndugu zake wawili Oyoo na Ojwang, ambao wamehamia Ufaransa.

Kwa hesabu za haraka haraka tu ili kubaini ni pesa ngapi zinalipwa, ada ya kila mwaka ya wanafunzi kwa miaka 17-18 ni Shilingi Milioni 1.08. Ikiwa mtoto wako ana makao shuleni, ada ya kila wiki ya kukodisha ni Shilingi 648,900, wakati usafiri kati ya Shilingi 112,200 – Shilingi 123,300.

Vile vile, hii ndio muundo wa ada ya shule ya Braeburn Mombasa;

Braeburn Mombasa school fees

Hivi ukajiuliza Akothee anazitoa wapi hizo hela zote?

Akothee ni msanii na analipwa kutumbuiza kwa matamasha nhcini ana nje ya nchi.

Image result for akothee and daughters

Akothee pia ana kampuni ya usafiri wa Akotheesafaris ambao ni chanzo kubwa cha hela.

Madam Boss yuko na baba watoto wake ambae ni mzungu na ana hela ajabu.

Hayo yote, Akothee hajawahi kuficha uhusiano wake na mzungu na anaishi maisha ya uwazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *