Mvua ya dakika ishirini imeleta uharibifu jijini Nairobi licha ya Gavana Mike Sonko kuahidi kwamba mifereji ya maji kwenye jiji na viunga vyake yako sawa kabla ya msimu wa mvua.
Wanajiji walitarajia kuwa juhudi za hivi karibu za serikali ya Sonko za kzibua mifereji ya maji zingesaidia kuhepuka madhara ya msiu uliopita.
Hata hivyo, mvua ya dakika chache iliweka ahadi ya Sonko kwa majaribio na sasa baadhi ya barabara hazipitiki.
Wakenya walikuwa wamepata afueni baada ya kuona mvua ikianza kunyesha kwa sehemu mbali mbali za nchi baada ya kukumbwa na kiangazi kwenye Kaunti nyingi.
Idara ya hali ya anga ilikuwa imetoa tahadhari kwamba mvua itanyesha kuanzia wiki hii, ikiangazia Magharibi mwa Kenya, Kati, na Kusini mwa bonde la ufa kama sehemu zitakazopata mvua nyngi.
Kauanti ya Nairobi na sehemu ya Kati ya nchi y Kenya pia ziliangaziwa kwa utabiri.