Magoha Aifunga Shule na Kuamuru Wanafunzi wote Kuhamishwa Shule Jirani (VIDEO)

Waziri wa elimu Profesa George Magoha Jumatano, Septemba 25, kwa hamaki alienda shule ya Kibra kwa lengo moja kuu.

Akiongea moja kwa moja kwenye runinga, Magoha alitangaza kufungwa kwa shule ya msingi ya St. Catherine Bombolulu ambayo kulingana na yeye iko kwenye hali ya hatari kama ilivyokuwa shule ya Precious Talent iliyopo Ng’ando Dagoretti.

“Nimekuwa kwenye majengo, nimeingia katika kila chumba, na hakuna tofauti kati ya majengo haya na yale yalioanguka ,” alikiri.

Magoha ambaye aliambatana na Katibu Mkuu wake, Belio Kipsang, aliamuru uhamisho wa wanafunzi 207 kutoka Bombolulu hadi shule jirani, Ayany Estate Primary.

“Watoto kutoka Bombululu watahamishiwa hadi shule hii (Ayang) kwa sababu ina nafasi za ziada,” alitangaza.

CS Magoha addressing the media after the closure of St. Catherine Bombolulu.

Magoha pia alifichua kuwa jengo hilo (shule ya Bombolulu) halikuwahi kuidhinishwa na mtu yeyote na majengo hayo pia hayakusajiliwa.

Katika hotuba yake, Magoha aliisihi jamii kuelewa kwamba wizara hiyo inafanya kazi kwa sababu ya maslahi ya watoto.

Wakati ziara ya ukaguzi wake, CS iligundua kuwa walimu katika shule ya Bombolulu hawakuwa wamesajiliwa na TSC, ikilinganishwa na Ayang ambayo ilikuwa na zaidi ya waalimu 27 waliosajiliwa.

Pia aliwapa uwezo maksusi maafisa kufunga shule yeyote amabyo ilikuwa katika hali sawia na St. Catherine Bombolulu.

“Kuanzia sasa hakuna mtu anayepaswa kuningojea mimi kufunga shule yoyote ambayo inaonekana kuwa katika hali mbaya sawia na tulioifunga. Nimewapa nguvu maafisa wangu kuzifunga shule hizo lakini kwa hali ya uadilifu,” alifafanua.

A collapsed Precious talent school in Ngando, that was closed by CS Professor George Magoha after it killed 7 pupils.

Hii inakuja siku mbili baada ya waziri kutangaza kufungwa kwa siku 4 kwa Shule ya Precious Talent huko eneo la Dagoretti Kusini ambapo jengo la ghorofa mbili lilianguka na kuwaua wanafunzi saba.

“Kwa sasa, tumewauliza wanafunzi kukaa nyumbani kwao kwa siku nne zijazo kwani tunaweka hatua za kutosha kuhakikisha usalama wao wanapo jifunza.

Magoha alitembelea eneo la mkasa  kutoa rambirambi kwa wakaazi na pia kuweka wazi hatua itakayochukuliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *