Baba mwenye Majonzi atoa Tamko baada ya Kumpoteza Binti Kwenye Shule ya Precious Talents

David Njeru, one of the parents who lost his child at Precious Talents school in Nairobi

Baba mwenye Majonzi, David Njeru, Jumatatu, Septemba 23, alielezea jinsi alivyoelezwa kuhusu kifo cha binti yake baada ya kuanguka kwa jengo la ghorofa mbili katika Shule ya Precious Talents jijini Nairobi.

Akiongea na runinga ya Citizen, Njeru alisema kwamba binti yake wa darasa la nane, Jamine Siti, alikuwa mmoja wa wanafunzi waliopoteza maisha wakati wa tukio la saa moja asubuhi.

Alielzea kwamba mkewe alimjulisha kuhusu tukio hilo la kusikitisha, alipokuwa njiani akienda kazini.

“Nilikwenda shuleni baada ya kukubaliana na mke wangu atamtafuta binti yetu kwenye zahanati zilizo karibu huku nikienda Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta.

“Kabla ya kufika KNH, hata hivyo, niliitwa na kuambiwa kwamba alikuwa ameaga dunia,” aliongeza kwa majonzi.

Njeru alielezea jinsi binti yake alikuwa mtendaji wa hali ya juu, na kuongeza kuwa alikuwa ameshikilia nafasi ya kwanza katika mtihani wake ya faharisi.

Kwa upande mwingine, alishukuru kuokolewa kwa mtoto wake wa darasa la saba.

The scene where a classroom with pupils collapsed on Monday, September 23, 2019

Siti alikuwa ni mmoja wa wanafunzi saba waliopoteza maisha katika janga hilo.

Evans Kamuri, daktari huko KNH, alisema kuwa wanafunzi wengi walikuwa wamepata nafuu, na kuongeza kuwa ni wawili tu kati yao walikuwa katika hali mbaya.

“Mvulana ana majeraha ya mapafu na figo. Msichana ana majeraha ya musuli laini hata hivyo hakuna uharibifu wa ndani,” alisema.

Ilipofika saa 2 usiku, wanafunzi 60 ambao walikuwa wanauguza majeraha yao hospitalini, walipatanishwa na wazazi wao.

Wanafunzi wanne bado wamelazwa hospitalini huku miili ya watoto waliofariki ikipelekwa katika hifadhi ya maiti ya City Mortuary

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *