Uhuru amkabidhi Matiang’i mamlaka zaidi kwa mara ya pili mwaka huu

Census

Rais Uhuru Kenyatta kwa mara nyingine ameongeza nguvu ya waziri wa Mambo ya Ndani, Fred Matiang’i akimuamrisha na kuratibu utoaji wa vipaumbele vya kitaifa.

Mabadiliko hayo, yaliyomo katika Agizo la Utendaji la Sita ya 2019, ni kufuata maagizo yaliyotolewa mwanzoni mwa mwaka kuweka Katibu wa Baraza la Mawaziri anayesimamia mashirika zaidi nchini.

“Ili kukuza ujumuishaji wa majukumu ya Usajili wa watu na kazi za Uhamiaji, Idara ya serikali ya Mambo ya Ndani na Idara ya serikali kwa Uhamiaji na Huduma za Raia imeunganishwa ili kuanzisha idara ya serikali ya Huduma za Mambo ya ndani na huduma za wananchi. Idara ya serikali ya Huduma za Mambo ya ndani na Raia itasimamiwa ndani ya Wizara ya Mambo ya ndani na Uratibu wa Serikali ya Kitaifa, ”inasema agizo hilo.

Image result for fred matiangi

Hii inampatia Waziri Mating’i nguvu zaidi nchini kwani hii ni moja wapo ya vyeo ambavyo amekabidhiwa tangu mwaka huu uanze.

Mwanzoni mwa mwaka Uhuru Kenyatta alimteua  Matiangi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Utekelezaji ya Maendeleo ya Jamii na Mawasiliano akimwweka kusimamia kazi ya mawaziri wote.

Wachanganuzi wa siasa wanasema kuwa hii ni kunpunguza makali ya naibu rais William Ruto ambaye amekuwa akiendesha shughuli hizo ambazo Matiang’i amepewa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *