Rais Uhuru Kenyatta Alhamisi alitangaza kuwa kumbukumbu ya 41 ya baba mwanzilishi wa nchi Mzee Jomo Kenyatta itakuwa ya mwisho.
Uhuru alisema makubaliano hayo yaliafikiwa baada ya mashauriano na familia nzima ya Kenyatta. Uhuru ameongeza kuwa kama familia watakuwa wakifanya sherehe ya kibinafsi kama wanafamilia kusonga mbele.
“Kama Rais, nimeshauriana na familia ya Mzee Kenyatta. Tumekubaliana kwa pamoja kwamba hii itakuwa sherehe ya mwisho ya kumbukumbu ya Mzee kwa njia hii,” alisema.
Alizungumza wakati katika Kanisa la Holy Family Basilica alipokuwa akiongoza taifa katika kumkumbuka za baba mwanzilishi wa taifa. Rais ameongeza kuwa nchi imesonga mbele katika miaka 41 na na kushuhudia mabadiliko na maboresho makubwa.
Pia aliwapa shukrani Marais wote wawili waliomtangulia kwa kuzingatia kama ibada maadhimisho ya Mzee Kenyatta bila kukosa.
Mzee Jomo Kenyatta alikufa mnamo Agosti 22, 1978.