Baa kufungwa kote nchini kwa ajili ya sensa- Matiang’i

Image result for fred matiangi

Waziri wa Mambo ya ndani, Fred Matiang’i, ameamuru kufungwa kwa baa zote wakati wa sensa.

Baa kote nchini zitabaki zimefungwa kwa siku mbili kuanzia Jumamosi 5:00 jioni kwa sababu ya kipindi cha sensa ya kitaifa.

Sensa ambayo inafanywa baada ya miaka kumi inafanywa Agosti 24 mpaka 31 mwaka huu.

Kulingana na KNBS, kupitia akaunti yao ya Twitter mapema mwezi huu, hii itakuwa sensa ya 8 kufanywa nchini Kenya.

Image result for census in kenya

Raia wanahimizwa kuwa ndani ya manyumba siku ya sensa ili kuhakikisha data sahihi inakusanywa wakati huo huo kuhakikisha kila mtu anashiriki.

“Habari itakayokusanywa ya sena itakuwa thabiti na KNBS inakuhakikishia kuwa itatumika kwa sababu za takwimu tu. Maafisa wote wa sensa wataapa kama inavyotakiwa na sheria. Maelezo ya kibinafsi hayatatolewa kwa umma, “ilihakikishia KNBS kupitia mtandao.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *