Wakenya kupigwa faini wakihepa sensa

Image result for census in kenya

Serikali iko tayari kufanya sensa ya sita ya kitaifa ya Kenya kutoka Agosti 24, 2019, na itaendelea hadi Agosti 31, 2019.

Kulingana na Sheria ya Takwimu ya 2006, mtu yeyote anayekosa sensa ana hatari ya kifungo cha mwaka moja au faini ya shilingi 100,000 au zote mbili.

Watu wote ambao watakuwa ndani ya mipaka ya Kenya kwenye usiku wa sensa (Agosti 24/25) watahesabiwa.

Hii ni pamoja na watu wanaopatikana katika manyumba zao, wale wanaosafiri, watu katika hoteli na nyumba za kulala za wageni, na taasisi kama hospitali na magereza, miongoni mwa wengine.

Sheria hiyo inasema kwamba watu watakaokataa kutoa habari yoyote au maelezo kama inavyotakiwa watachukuliwa kuwa wamefanya kosa.

Sensa ya mwaka huu ni ya kwanza tangu kutangazwa kwa katiba ya 2010 na ya kwanza kufanywa kwa kutumia vifaa vya kidigitali ambavyo vinahakikisha usahihi, kasi na usalama wa data.

Ikiwezekana ifikapo Agosti 31 bado haujahesabiwa, nambari isiyo na malipo itapewa ili kuwasiliana na KNBS kutuma waendesha shughuli hiyo ili kuhesabiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *