Je, Serikali inampotezea Bobi Wine muda kwa kesi isiyo sahihi?

Related image

Mbunge wa Kyandondo Masahariki Bobi Wine siku ya jana  alijitokeza katika korti ya Barabara ya Buganda kwa kesi nyingine inayoaminika kubuniwa na serikali dhidi yake.

Bobi Wine kwa wakati huu, ameshutumiwa kwa kesi ya kuhusika katika maandamano dhidi ya kodi ya mitandao ya kijamii inayokandamiza.

Walakini, korti ya barabara ya Buganda iliahirisha kesi hiyo hadi tarehe 19 Septemba, 2019 ili kutoa muda wa mashtaka ya kuandaa mashahidi na ushahidi.

Image result for bobi wine in court

Wakati ni jukumu la serikali kudumisha sheria na utaratibu, imekuwa tabia ya Museveni na NRM kucheza mchezo wa paka na panya katika siasa dhidi ya wale wanaompinga.

Serikali inapiga kila aina ya mashtaka ili kupoteza muda wapinzani wake na kuhakikisha mifuko yao yamekuwa kavu kwa njia ya ada ya kisheria.

Wengi wameshutumu serikali kwa kutumia huu mfumo wa kisheria ili kuhangaisha wapinzani wa Museveni na pia kwa kuhairisha kesi.

Bobi Wine anawania kiti cha urais cha mwaka wa 2021 na serikali inafanya juu chini kuhakikisha hajapata nafasi ya kufanya kampeni zake.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *