Tubadilishe mitindo zetu za maisha ili kupigana na saratani- Uhuru

Image result for uhuru kenyatta in bomet

Rais Uhuru Kenyatta ameonya Wakenya kuacha kununua vyakula vilivyotayarishwa kutoka maduka makubwa na badala yake kurudi kwa chakula cha jadi ili kuzuia saratani.

Uhuru aliwahimiza pia kuachana na mitindo za maisha ya wazungu na kurudi kwenye mtindo wa kitamaduni.

Rais alisema saratani ilikuwa jambo geni sana barani Afrika lakini sasa kimekuwa kitu cha kawaida watu wanapoacha vyakula vya kiafrika.

Image result for uhuru kenyatta in bomet

Rais alizungumza wakati wa kumbukumbu ya marehemu gavana Joyce Laboso Ijumaa kwenye Uwanja wa Bomet Green Stadium.

Kwa wale wanaougua saratani, Uhuru aliahidi kuongeza bajeti iliyowekwa kwa matibabu ya saratani ili wagonjwa waweze kupata matibabu bora nchini.

“Kufikia Septemba serikali yangu itahakikisha kuwa kuna kituo cha chemotherapy katika Hospitali ya Longisa, Bomet kwa matibabu ya saratani, “Uhuru alisema.

Image result for Joyce Laboso and DP Ruto

Rais pia alisema kuwa vituo vitatu vya radiolojia vitaundwa kitaifa huko Garissa, Mombasa na Nakuru kusaidia katika matibabu ya saratani.

Uhuru alisema ataboresha Hospitali ya Rufaa ya Moi, Eldoret kuwa moja ya hospitali za matibabu ya saratani na kituo cha mafunzo.

Rais aliahidi kuandaa na kufungua Hospitali ya Chuo Kikuu cha Kenyatta mnamo Septemba kwa matibabu sahihi ya saratani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *