Dondoo za asubuhi: Vodacom kikaongoni kuvujisha mawasiliano, Karume: Mwakani mtapewa risasi muwatandike wananchi; Wadau waja juu vitambulisho vya Polisi wa Kabendera

Habari ya Asubuhi mdau wa Opera News!

Tunatumaini umeamka salama

Nukuu: Kila siku ni mwanzo mpya, vuta pumzi, tabasamu na kisha anza upya!

Na wakati unaianza siku mpya tunakukaribisha tena kwenye dawati letu la  OPERA NEWS kukupa habari tatu za moto zinazotikisa kila siku asubuhi.

Vodacom ndani ya sakata zito la kuvujisha siri za wateja, unajua wananchi wamesema nini? Fatma Karume nae awaahidi jeshi la polisi magari ya washawasha unajua kwa nini kasema hivyo? Je wajua nini kimewapata askari walioenda kumkamata Kabendera bila kutoa kitambulisho?

Soma hapa chini kujua zaidi kuhusu stori zinazobamba leo;

VODACOM YALAUMIWA KUVUJISHA MAWASILIANO YA WATEJA, WATISHIA KUWAKIMBIA

Kampuni ya Vodacom yalalamikiwa kuvujisha mawasiliano ya wateja wake wengine watishia kuwakimbia

Baadhi ya wadau wa mitandao ya kijamii wameishambuli vikali kampuni ya simu za mikononi Vodacom kwa kitendo cha kuvujisha mawasiliano ya wateja kinyume cha sheria.

Wakitoa maoni yao wameeleza kuwa kampuni hiyo sio mara ya kwanza kulalamikiwa kutoa siri za wateja huku wengine wakitishia kuhama kutumia line ya Vodacom.

Soma Zaidi>>>  

WAKILI FATUMA: MWAKANI MTAPEWA GARI ZA WASHAWASHA, VIRUNGU, RISASI ILI MUWATANDIKE VIZURI WANANCHI

Tokeo la picha la fatma karume

Wakili wa kujitegemea, Fatuma Karume ameliambia jeshi la polisi wasiwe na hofu mwakani watanunuliwa gari za maji ya washa washa, virungu, ngao, kofia ngumu, risasi na bunduki ili wawatandike vizuri wananchi.

Soma Zaidi>>>

WADAU WAHOJI KWA NINI ASKARI WALIOMKAMATA KABENDERA WALIGOMA KUONYESHA VITAMBULISHO

Tokeo la picha la kabendera

Jeshi la polisi likiwa linaendelea na mahojiano na mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera baadhi ya watu wamehoji iweje askari hao wagome kutoa vitambulisho vyao vya kazi.

Kadhalika, imedaiwa kuwa mwandishi huyo ambaye huandika habari za ndani na nje ya nchi alishawahi kuhojiwa uraia wake na kuonekana hana tatizo.

Soma Zaidi>>>

Tokeo la picha la ijue Homa ya Ini

Katika kumalizia dondoo zetu, tukugusie kwa ufupi kuhusu ugonjwa hatari wa Homa ya Ini (Hepatitis). Madakatari  wanasema ini hufanya kazi zaidi ya 500, moja ya kazi kuu ni kuchuja na kuondoa sumu kwenye damu.

Homa ya Ini ni ugonjwa unaosababishwa na Virusi vinavyoshambulia Ini au wakati mwingine inatokea baada ya ini kupata madhara kutokana na sumu mbalimbali (hasa pombe, madawa fulani na mimea), husababishwa pia na maambukizi mengine na magonjwa ya kingamwili

Virusi vinavyosababisha Homa ya Ini vipo vya aina tano, yaani A, B, C,D, E. Leo tutaangalia vyanzo vya homa ya Ini inayosababishwa na virusi aina  B na C. Virusi hivi vimetajwa kuwa ni hatari zaidi ya virusi vya Ukimwi.

Kama ulivyo Ukimwi, ugonjwa huu huambukizwa kwa njia ya kujamiiana, mate au mwingiliano wowote ule wa damu. Virusi vya homa ya ini pia huweza kusambazwa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kuzaliwa au kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa njia ya kuongezeana damu yenye virusi.

Naam, kesho panapo majaliwa tutaangazia dalili, vyanzo vingine vya Homa ya Ini na jinsi gani unakuwa hatarini kupata ugonjwa huu. Jiwekee utatibu wa kuchunguza afya yako

Ni hayo tu kwa asubuhi ya leo kutoka Opera News, tuandikie maoni yako hapo chini..

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *