Wahamasishaji wawili walioteuliwa na People Power wakataa ofa ya Bobi Wine

Image result for people power announces bid for presidency

Muda chache baada ya chama cha People Power kinachoongozwa na mbunge wa Kyandondo Mashariki, BobiWine kutangaza azimio lake la urais wa mwaka wa 2021 na waratibu na wahamasishaji, watu wawili wameongezeka kupinga uamuzi huo.

Muundo huo inajumuisha baraza la ushauri, mratibu wa mkoa, baraza la uongozi ambao watashughulikia kampeni za People Power kwenye kinyanganyiro cha uchaguzi kwenye nchi nzima.

Mbunge wa kaunti ya Jie Adome Bildad Moses ambaye ako kwa chama tawala, National Resistance Movement (NRM) alikataa kujua kuwa aliteuliwa kuongoza uratibu wa People Power kwenye eneo la Karamoja.

Related image

Odome aliyekiri kuwa alipata habari hiyo kwenye mtandao wa kijamii alikuwa na haya ya kusema;

“Ambapo pia ni haki yangu kujiunga na vyama vingine vya siasa, pia ni haki yangu kulindwa kutokana na hali ambazo zinaweza kuhusishwa na jukumu langu kama mbunge kutoka NRM. Nitaomba kujua ni nini People Power inasimama na nini wanataka nisaidie ambayo inaweza kusaidia watu ambao mimi huongoza. Kwa hayo machache, ningependa kusema kuwa siwezi jiunga na vitu ambavyo sioni mwangaza kwayo,”

Mwingine pia aliyeteuliwa ni Elakuna Isaac (FDC) ambaye ni msemaji wa munispaa ya Soroti, ambaye anasema kuteuliwa kwake kuwa mratibu wa Teso, hakuhusishwa.

Image result for Elakuna Isaac

“Nimeliona jina langu likisambaa kwa mtandao na baadhi ya marafiki wa karibu wakinipongeza kwa kuteuliwa. Hii ni kitu nzuri lakini sikuhusishwa, ningependa kusema kinagaubaga kwamba chama changu ni FDC na sina nia ya kukibadilisha,” alisema kwa taarifa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *