Wiki chache baada ya kumuonya Tanasha juu ya madai ya utelekezaji wa majukumu kwa msanii wa Bongo, Diamond Platinumz, Zari amefichua kuwa hajawahi kutana na Tanasha lakini huwa anamwona kwenye sehemu ya maoni mtandaoni.
“Sijawahi mtafuta Tanasha na sikuwahi mjua mpaka watu walipoanza kunitaja wakidai kwamba Tanasha alikuwa kwenye mtandao ya kwangu akiuza na kutangaza vitu vyake. Sijawahi mwona lakini alikuwa kwa sehemu ya maoni kwenye Instagram yangu ndo siku nilliliona jina lake,” alisema Zari kwenye Milard Ayo.
Mama wa watano aliongezea kuwa Tanasha alipanda cheo kutoka kwa kutoa maoni kwa sehemu ya mtandao yake hadi kuwa mchuma wa Diamond.
“Watu wanaishi ndoto zao, wanaona ndoto zao zikitimia. Kili kitu kinawezekana, ota na itafanyika,” alisema.
Hassan pia alisema kuwa maoni yake kwa ujauzito wa Tanasha ilikuwa imezua vurugu. Alisema kuwa hakusema kwa nia mbaya bali alikuwa anampa ushauri tu asije akapatikana ghafla.
Alipoulizwa kuhusu alichokiana kwa tamasha la Great Gatsby, alisema kuwa hakukuwa na chochote kipya kwenye siku hiyo maanake alikuwa amefanyiwa hadi na tamasha kubwa kushinda hiyo.
“Ukiona hiyo Diamond alifanya sio geni, ni vitu anavirudia tu,” Mama Tee alisema.