Bosi Lady AKothee amewashangaza mashabiki wake baada ya kufichua kinagaubaga kwanga anauguza jeraha la moyo kwa mara nyingine. Mama wa watano huwa hababaiki na maisha yake kwenye wazi lakini kimya alichotunza kwa mpenzi wake ni jambo jipya.
Akothee amekuwa na shughuli nyingi kati ya kulea wana wake na biashara zake kitu ambacho hakuna yeyote angetambua kuwa ana mpenzi.
“Tumeachana na mpenzi wangu. usiniunile ni mgani, we jua tu imekwisha, juu nilikata mikutano yetu kwa sababu nafaa kufanya kazi wikendi hii tuliyopanga”.
Amemshukuru kwa wakati waliokuwa nao pamoja kama kwamba alifurahi sana.
“shukrani nyingi, nilifurahia wakati tuliokuwa nawe na nitaikumbuka milele, nitakukosa, lakini nitakula ugali wangu na kukusahau hivi karibuni π.”
Inaonekana kama madam bosi amechukua mkondo wa Zari ya kujificha nyuso za bae na utambulisho kutoka kwa Instagram.