Sikumwacha Diamond kwa sababu ya kudanganya- Zari Hassan akiri

Image result for diamond and zari

Mwanabiashara Zari Hassan kwa mara ya kwanza ameyaweka wazi kiini na shinikizo kilichompelekea kumwacha staa wa Bongo, Diamond Platinumz.

Zari alikiri kuwa hapakuwa na heshima kwenye ndoa yao na kwamba Diamond sio mtu alikuja kumheshimu na kikapelekea kumwacha.

Akizungumza na Millard Ayo wa Tanzania, aliongezea kuwa hakumwacha Diamond kwa msingi wa kufanya mapenzi nje ya ndoa.

“Mimi kuachana na Diamond haikuwa sababu ya udanganyifu, wanaume wanafanya hivo kila wakatti. Ni kwa sababu wanakuheshimu sana ata wasikuambie. Lakini kwa Naseed ilikuwa dharau. Unaleta wasichana kwenye mitaa na mnatumia kitando chetu na watoto. Na pia hakutumia mipira za kujisitiri.Hakukuwa na heshima kabisa.”

Image result for diamond and zari

Zari alielezea jinsi Diamond Platinumz alikuwa anakana kufanya mapenzi na wasichana wa mitaani na hakuwahi kukiri kumdharau Mama Tee.

Diamond hivi majuzi alisema kwenye radio ya Wasafi kuwa Zari alimzuia kuwaona wana wake Tiffany na Nillan na kubaki kuwaona kwenye mtandao.

Akilijibu hili, Mama Tee alisema hajawahi ongea na Diamond kwa miezi tisa na hivyo hivyo kwa watoto wao.

“Mimi Sijaongea na Nasseb kwa miezi tisa, hajaona watoto miezi tisa, hajaongea na watoto miezi tisa. So hiyo sio ukweli. Unajua vile tumeachana na Nasseb, tunafaa kuongea mambo fulani, Mpaka sasa watu wanasema ooh una roho mbaya umemkataza Naseeb kuona watoto. Niliwachana na Naseeb kama yeye na sikumwambia wachana na watoto wako” aliongeza Zari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *