Mambo yanaendelea kuenda segemnege kwa makampuni zinazoendesha biashara ya michezo za kamari. Hii ni baada ya korti kutupilia mbali mswada wao dhidi ya tume ya udhiti wa michezo za bahati nasibu (BCLB).
Advanced Gaming Limited, ambayo ni moja kati ya makampuni, ilikuwa imeomba korti kuizimamisha amri la BCLB wa kuisimamisha kampuni hiyo wiki jana.
Makampuni yaliafikiana kungoja hadi kesi dhidi yao isikizwe kwenye mahakama kuhusu kufungwa kwa biashara zao.
Jaji Weldon Korir, hata hivyo, alikataa kutoa amri za kihafidhina akisema kwamba hakuona haja.
Kesi hiyo imehairishwa hadi tarehe 26 mwezi huu wa Julai.
Makampuni 27 kwa sasa yamefungwa na mfumo wa malipo wa Paybill kuvunjiliwa mbali huku wakurugenzi 17 ambao ni wageni wakiamrishwa kuhamishwa kutoka Kenya kwa mujibu wa Waziri wa ndani Fred Matang’i.