Pigo kwa kampuni za kamari baada ya Matiang’i kuwahamisha wakurugenzi

Image result for fred matiangi to betting firms

Waziri Fred Matiang’i ameamrisha kuhamishwa kwa wageni 17 ambao ni wakurugenzi wa maka puni ya michezo ya kamari. Amri hiyo inafaa kuchukuliwa hatua mara moja.

Sekta hiyo yenye mamilioni ya pesa imepata pigo hii baada ya kutolewa kwa malipo ya Mpesa na Airtel.

Wiki jana, bodi ya leseni ya michezo za kamari (BCLB) ilinyima leseni makampuni 27 ambazo zilikuwa zinaendeshwa nchini kwa tuhuma za kugaidi kulipa kodi miongoni mwa makosa mengine.

Jumatatu wiki hii, benki kuu ya Kenya ilitoa agizo kwa BCLB kuchunguza akaunti za kamuni hizo 27 ambazo zilinyimwa leseni.

Image result for sportpesa

“Tunataka kuwajulisha kwamba leseni za makampuni ya kamari zifuatazo hazijapata upya hadi zinapokutana na mahitaji mapya ya kisasa na matokeo ya kuendelea kufanya kazi na tutatoa ujumbe baadye tukiamua ikiwa ni sahihi ya kushikilia leseni kutoka kwa bodi hii. Kwa hiyo, tunakuomba kusimamisha bili zao za kulipa na nambari fupi mpaka unaposhauriwa,” inasoma barua ya Julai 10, 2019.

Kwa kushangaza, hatua ya kufukuza wageni inakuja wakati ambapo Mbunge wa Starehe Charles Njagua almaarufu Jaguar anakabiliwa na mashtaka mahakamani kwa kutishia wageni.

Image result for jaguar arrested

Rais Kenyatta na Matiang’i walimsuta Jaguar kwa kutofautiana naye na kilichompelekea Uhuru kusafiri hadi Tanzania kumpata Pombe na kuomba msamaha.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *