Zari awaomba mashabiki wake wamsaidie kumtuliza ‘wazimu’ Akothee

Image result for Zari and akothee

Tangu mwanamziki na mwanabiashara wa kike Akothee alipopata alama ya bluu kuashiria kuthibitishwa kwenye mtandao wa Instagramu, wafuasi na familia yake hawajakuwa na amani.

Imepita karibu wiki moja baada ya Akothee kuthibitishwa na Instagramu na mama wa watano hajatulia ata kidogo maana ya kusherehekea hatua hiyo katika maisha.

Akothee pia aliwaonya wafuasi wake wakiwemo watoto wake ambao hawajathibitishwa kwa kutomsemezea maanake hawana idhini yoyote.

Baada ya kuitwika video hiyo kwenye mtandao, mwenzake kutoka Uganda, Zari Bosslady alikiri kuwa Akothee amekuwa akimpuuza na kutoshika wito zake alipompigia.

Image result for akothee

Zari aliwaomba mashabiki wake wamsaidie kujua jinsi ya kushughulika na mwanmke mwenda wazimu kama Akothee.

“Je, unaweza kunipigia sasa, ndo maana hukuwa unanijibu? Mtu anifunze jinsi ya kushughulikia wanawake wazimu,” alilaani Zari.

Akothee na Zari wanaandaa mkutano mkubwa wa wanawake ambayo itafanyika pale Mombasa. Zari amesikitika kuona kuwa mshirika wake hashiki simu zake na wanapaswa kumaliza maandalizi.

 

View this post on Instagram

 

Dont talk to me if you are not Veryfyed 👨‍💻👨‍💻 ,I am bisi plis @rue.baby @veshashaillan @fancy_makadia

A post shared by AKOTHEE KENYA (@akotheekenya) on

Akothee kwa upande wake angali anasherehekea ubabe wa kupata alama ya bluu ambayo ni tofauti kiasi ni ile ya Whatsapp.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *