Mwana wa Anyang Nyong’o awasisimua wengi na rinda nzuri

Related image

Kwenye zilizala za ulimwengu wa mtindo wiki hii tunaelekea kwa mwana wa gavana Anyang Nyong’o.

Peter Junior Nyong’o, mwana wa gavana wa Kisumu Anyang Nyong’o ni mwanamtindo mzuri na ugwiji wake wa mavazi ya kipekee daima unaacha wengi vinywa wazi.

Kutoka kuvaa mavazi ya wanawake hadi kushiilia maua, mwanamtindo huyo huwa habahatishi ata kidogo na kugonga vichwa vya habari.

Image result for peter junior nyongo

Wikendi iliyopita, alihudhuria harusi moja akiwa amevaa gauni refu iliyo na alama ya kiafrika. Aliambatanisha muonekano hiyo na saa kwa mkono huku ameshikilia ua nyeupe.

Cha kushangaza zaidi ni kwamba watu waliokuwa na ya kusema walimpongeza kwa kuonekana nadhifu kwa vazi hilo la wanawake.

“FL🌺WER B🌸Y AKA JUNELOPE JONES. FIT BY @ZEROBYZAWADI,” aliweka maelezo picha hiyo.

Wengi wamekuwa wakimdihaki kwa muenokano wake huku wengi wakishuku kuwa anapenda jinsia ya kike.

Zero kutoka Zawadi pia inajulikana kuwa ni kampuni ya dadake mdogo Zawadi Nyong’o.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *