Bwenyenye Charles Mbire afichua siri za Benki ya Uganda, asema kilichokuwa ndani ya ndege

Image result for charles mbire

Mabwenyenye Charles Mbire na Omar Mandela wamekuwa wakifanyiwa mahojiano na maafisa wa polisi wa uchunguzi na jinai kutoka Jumanne.

Charles Mbire ambaye ni mwenyekiti wa MTN Uganda na aliyewekwa kwa gazeti la Forbes kama mmoja wa watu tajiri Ugnada mwaka wa 2012 na mwenzake Mandela ambaye ni bosi wa City Oil Petrol Stations waliitwa na msemaji wa serikali Ofwondo Opondo kwa madai ya kuwa na noti mpya za Uganda kwa ndege ya BOU.

Image result for charles mbire and BOU plane

Kashfa hii ilianza baada ya maafisa wa mamlaka ya mapato nchini Uganda kusisitiza kuchunguza kilichokuwa kwa hilo ndege.

Akiongelea madai hayo ya noti mpya kupatikana kwa ndege, Mbire alisema kuwa kilichokuwa kwa ndege hilo ni kibuyu cha rangi alichokileta ili kupaka meli yake.

Related image

“Nilinunua lita ishirini ya rangi aina ya ‘adhesive glue’ ilikupaka meli yangu, nilitumia kampuni ya Allied Cargona jinsi ilivyoletwa siijui,” Mbire alisema.

Hata hivyo, maafisa hao walisema mabwenyenye sio washukiwa bali watasaidia kwa uchunguzi wa mzigo ulioletwa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *