Waziri atangaza neema kwa wakulima wa mahindi

 

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga ametangaza neema ya kuanza kununua mahindi nchini kutokana na kupata masoko makubwa kwenye nchi za kusini mwa Tanzania ambazo zinahitaji tani milioni moja.

Wakala wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko(CPB) wataanza kununua na kukusanya mahindi kutoka kwa wakulima.

Hasunga alitoa tamko hilo bungeni jana alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti maalum (Chadema), Aida Khenani ambaye alihoji serikali imejipangaje mwaka huu katika ununuzi wa mahindi kwa kuwa hivi sasa ni msimu wa mavuno.

Akijibu swali hilo, Hasunga alikiri kuwa kwenye msimu uliopita wa kilimo kulikuwa na changamoto ya masoko ya zao hilo lakini serikali imekuwa ikihakikisha inatafuta masoko.

“Hivi sasa tumepata masoko makubwa ya mahindi nchi za kusini, Hivi sasa Rwanda wanahitaji zaidi ya tani 100,000, Burundi wanahitaji zaidi ya tani 100,000, Zimbabwe wanahitaji tani 800,000 za mahindi na nchi nyingine nyingi zinahitaji kwa wingi,”alisema.

 

Hasunga alisema hivi sasa soko la mahindi ni kubwa sana na kutoa wito kwa wakulima wa mahindi kujitokeza kueleza kiasi alichonacho ili kushirikiana na serikali.

Aidha alisema taasisi nyingine ambayo imepewa jukumu kupeleka mahindi nchini Zimbabwe itaanza kununua mahindi wiki hii.

Aliwataka wakulima kukaa mkao wa kula kwa kuwa hivi sasa ni wakati wa kula mkate mzuri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *