QUEEN DARLEEN AELEZEA KWANINI NYIMBO ZAKE HAZIFANYI VIZURI YOUTUBE

Mwanamuziki  kutoka lebo ya WCB Queen Darleen amefunguka juu ya nyimbo zake kutofanya vizuri katika mtandao wa Youtube llicha ya kufanya promo kubwa ya muziki wake.

Akizungumza na mtandao wa Dizzimonline ,Queen Darleen amekiri kuwa baadhi ya nyimbo zake zimekua hazifanyi vizuri katika mtandao wa Youtube ikilinganishwa na wasanii wengine wa WCB “Bado Youtube yangu haijakaaa vizuri kihivyo” aliongeza msanii huo anayetamba na audio yake ya ‘tawire’

Miaka ya hivi karibuni baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva kama Baraka Da Prince waliweka bayana kuchezewa faulu katika mtandao huo hivyo kusababisha nyimbo zake kutofanya vizuri kwa upande wake Queen Darleen alipoulizwa juu ya ya uwezekano huu alijibu “haiwezekani Youtube kuchezewa kwani iko sehemu salama na Youtube wanaitambua”

Katika akaunti yake rasmi ya msanii huyo katika mtandao wa Youtube ana subscribers 39,060 idadi ambayo ni ndogo kwa msanii kutoka lebo hiyo ya Wasafi na wimbo.

 

IDADI YA SUBSCRIBERS  KWA WASANII KUTOKA WCB.

  1. Diamond Platnumz               1,942,740
  2. Harmonize                               952,997
  3. Rayvanny                                  872,909
  4. Mbosso                                     539,423
  5. Lavalava                                    386,818
  6. Queen Darleen                          39,060

Leave A Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *