Azam TV waomba radhi kushindwa kuonesha mechi za Play off

Gari la kurushia matangazo la Azam TV

Kufuatia kushindishikana kurusha mubashara michezo ya Playoff kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wao, Azam TV wamewaomba radhi wateja wao kwa tukio hilo.

Jana Azam TV walikuwa waoneshe michezo miwili ya Playoff ambayo ilikuwa kati ya Kagera Sugar dhidi ya Pamba pamoja na ule wa Geita dhidi ya Mwadui lakini yote ikashindikana kuoneshwa

Azam TV, kupitia ukurasa wao rasmi wa Instagram wameandikana hivi:-

“Mpendwa mteja wetu, tumelazimika kuondoa magari ya matangazo katika viwanja viwili vya Geita & Nyamagana baada ya kutokea sintofahamu na vurugu juu ya urushwaji live wa mechi mbili za FDL Playoff.

“Awali, Azam Media Ltd iliombwa na TPLB kusaidia kuonyesha live mechi hizo ili kudhibiti vitendo vya hujuma, Azam TV ilikubali ombi hilo na kufanya maandalizi yote ikiwa ni pamoja na kusafirisha magari ya matangazo mpaka viwanja husika kwa kuzingatia umuhimu wa ombi la TPLB.

Wachezaji wa Kagera Sugar wakishangilia goli katika moja ya michezo yao (Picha/maktaba)

“Msimamo wa Azam Media Ltd ni kutenda haki na usawa kwa ama kuonesha mechi zote nne au kuacha kabisa kuonesha mechi hizo. Baada ya Azam Media Ltd kuondoa magari yetu na kuanza safari kurudi DSM, tumepokea ombi jipya toka TPLB kuwa mechi hizo hazitafanyika leo na wametuomba tubakie na kuzionesha tena hapo kesho.

“Azam Media Ltd imekubali ombi hilo kwa maana hiyo mchezo kati ya Pamba na Kagera utaruka Kwenye chaneli ya Azam Sports 2 hapo kesho (leo) saa 10 jioni na mchezo kati ya Geita Gold na Mwadui FC utaruka Azam Sports HD kesho saa 10 jioni.

“Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *