Aussems kushusha ‘mashine’ mpya tano Simba

Kufuatia kikosi chake kuwa na mapungufu kadhaa katika idara ya ulinzi hususani kwenye michezo ya kimataifa, Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba Mbelgiji, Patrick Aussems amesema kuwa anatarajia kukisuka kikosi chake kwa umakini mkubwa ili kiweze kutoa ushindani mkubwa kwenye Ligi Kuu na michuano ya kimataifa, hivyo ameahidi kuleta nyota watano ili kuleta changamoto mpya ndani ya kikosi hicho.

Aussems amekuwa na msimu mzuri kwenye klabu ya Simba baada ya kiongoza kikosi hicho kutwaa ubingwa msimu huu akiwa na pointi 93 pamoja na kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni sehemu ya mkataba wake mpya kutetea ubingwa huo.

“KIkosi changu kimekuwa na tatizo kubwa hasa kwenye upande wa beki ambapo Shomari Kapombe amekuwa akisumbuliwa na majeruhi hivyo ni lazima niwe na mbadala wake msimu unaofuata pia kwa ajili ya michuano ya kimataifa.

“Wachezaji watano ama wanne wa kigeni watakuwa muhimu kuwapata, kwa sasa nimekabidhi ripoti nasuburi tu wakati ufike,” amesema.

Aussems amefanikiwa kuitengeza Simba inayocheza soka la kuvutia kwa pasi fupifupi zinazoambata na kasi hali iliyowapa shida wapinzani wengi wa Simba katika Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na michuano mingine ya hapa ndani.

Msimu ujao atakuwa na kibarua kingine cha kuiongoza Simba baada ya kupewa mkataba mpya ikiwa na pamoja na kuifikisha Simba hatua ya mbali zaidi katika michuano ya kimataifa zaidi ya msimu huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *