Fainali ya Esperance na Wydad yawakalisha CAF chini kwa dharura

Kufuatia hali ya sintofahamu katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kati ya Esperance de Tunis ya Tunisia na Wydad Casablanca ya Morocco, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeitisha kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji ili kujadili mchezo huo.

Rais wa Shirikisho hilo Ahmad Ahmad ameitisha kikao hicho cha dharura cha Kamati ya Utendaji ili kujadili mapungufu yaliyotokea ambayo kimsingi yametia doa kubwa sana katika tasnia ya soka barani Afrika, ikizingatiwa kuwa mchezo huo ulikuwa ukionekana dunia nzima.

Mei 31 nchini Tunisia kati ya wenyeji Esperance de Tunis na Wydad Casablanca ya Morocco mchezo uliisha kwa sintofahamu kufuatia klabu ya Wydad kugomea kuendelea na mchezo baada ya bao lao la kusawazisha kukataliwa katika dakika ya 62 ya mchezo.

Taarifa ya CAF imesema kuwa kikao hicho kitafanyika Juni 4, ambapo ajenda kuu itakuwa ni juu ya sheria zanazopaswa katika kutatua sintofahamu ya mchezo huo.

Kwenye mchezo huo, Wydad walisawazisha bao, ambalo lingeufanya mchezo kuwa sare ya 1-1 lakini mwamuzi alikataa bao hilo na halikurudiwa katika teknolojia ya usaidizi wa video VAR kwa kile mwamuzi alichokidai kuwa mashine kuharibika.

Baada ya Wydad kugoma kuendelea na mchezo, mwamuzi alimaliza mchezo na kuipa ushindi wa bao 1-0 klabu ya Esperance pamoja na ubingwa wa michuano hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *