Anthony Joshua apigwa ‘TKO’, ameacha ujumbe huu kwa mbabe wake

Bondia ‘Kibonge’ Andy Ruiz Jr kutoka Mexico ameishangaza dunia kwa kumtwanga bingwa wa uzito wa juu wa masumbwi duniani Anthony Joshua katika mpambano uliofanyika alfajiri ya leo huko New York Marekani.
.
Andy Ruiz ambaye alikuwa hapewi nafasi kabisa ya kumpiga Joshua ambaye ambaye hajawahi kupoteza pambano hata moja mpaka sasa.

Mchezo huo uliopigwa alfajiri ya kuamkia leo Juni 2 nchini Marekani, Umepelekea Joshua kupoteza mikanda yake ya ubingwa wa dunia ya WBA, WBO, IBF na IBO.

Ameingia katika historia ya kuwa bondia wa kwanza wa Mexico kushinda mataji makubwa ya ndondi duniani kwa ushindi wake wa Technical Knock Out ‘TKO’ katika raundi ya 7 ya mchezo.


Baada ya mchezo huo Joshua ameiambia Sky Sports: “Nimepigwa na mpambanaji kweli kweli.”

“Ni jambo la kuvutia kujua atafika mbali kiasi gani, lakini yote hii ni sehemu ya safari.

“Kwa sasa yeye ndiyo bingwa, nitarejea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *