Idadi ya wagonjwa wa kipindupindu yaongezeka Dar

 

Moja ya sababu iliyotajwa ya kuwepo kwa wagonjwa wengi wa Kipindupindi katika Wilaya ya Temeke ni baadhi ya wananchi kutiririsha maji yenye kinyesi.

Hayo yalisemwa leo na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Yudas Ndugile wakati akitoa taarifa ya ugonjwa wa kipindupindu, alisema idadi imeongezeka na hadi sasa jumla ya wagonjwa 55 wametibiwa jijini.
Alisema wilaya ya Temeke inaongoza kuwa na wagonjwa wengi waliotibiwa wamefikia idadi ya 34 na waliolazwa kambini wapo sita.
“Leo kwa wilaya ya Temeke tumepokea wagonjwa wapya watatu na kufanya idadi hiyo kufikia 34 kwa kuwatibu wapo wanaopatiwa huduma na kuondoka na wengine kulazwa,” alisema
Alisema kwa Wilaya ya Ilala jumla ya wagonjwa 19 wametibiwa na waliolazwa ni watano.
Dk. Ndugile alisema shida kubwa ambayo wameibaini katika hayo maeneo yenye wagonjwa wengi ni utiririshaji wa maji yenye kinyesi hali iliyosababishia kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa huo.

“Haya maeneo wengine wanatumia maji ya visima wanavyotiririsha maji yenye kinyesi kuna uwezekano mkubwa yakaingia katika visima hivyo kwa sababu kuna visima vingine ni vifupi ama mtoto akachezea hayo maji na kupata maambukizi ya ugonjwa,” alisema
Aidha, alisema ni vizuri wananchi wakachukua tahadhari mapema na kuacha kutiririsha maji taka na mama lishe kuhakikisha chakuka chao wanatengeneza katika mazingira salama kwa kuzingatia afya ya mlaji.
“Hawa mama lishe wawahimize wateja kunawa mikono yao kwa sabuni kabla ya kula chakula maana huu ugonjwa unasababishwa na uchafu ni muhimu kuzingatia suala nzima la usafi,”

Leave A Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *