Simba kimya kimya usajili, waanza na hawa hapa

Francis Kahata

Baada ya mahasimu wao wakubwa Yanga kuanza usajili kwa kasi kubwa kuelekea msimu ujao wa Ligi na kufanikiwa kuwanasa nyota kadhaa, inaelezwa Wekundu wa Msimbazi, Simba nao wameanza kimya kimya suala la usajili ili kukisuka kikosi chao kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, michuano mingine ya ndani na ile ya kimataifa.

Taarifa za chini ya kapeti zinaeleza kuwa tayari Simba wamefanikiwa kunasa saini ya nyota na nahodha wa Yanga Ibrahim Ajibu ambaye inaelezwa amesaini miaka miwili wakati huo huo wakiwa katika hatua za mwisho kumsainisha nyota wa Gor Mahia na timu ya taifa ya Kenya Francis Kahata pamoja beki kisiki wa kulia wa Lipuli Haruna Shamte.

Ibrahim Ajibu

Inadaiwa kuwa fedha ya usajili pekee ambayo amepewa ni Sh 90m huku mshahara ambao atakuwa akilipwa kwa mwezi ni Sh 7m, hivyo kwa kipindi chote cha miaka miwili atakayokuwa na Simba jumla ya mshahara wake utakuwa ni Sh 168 milioni.

“Kwa hiyo ukizijumlisha fedha hizo za mshahara ambazo atalipwa kwa miaka hiyo miwili pamoja na zile za usajili utangundua kuwa jumla ya fedha atakazochukua akiwa Simba ni Sh 258m.

“Hata hivyo mpaka sasa ameshalipwa Sh 80m, ambapo tayari ameshaanza kuzifanyia kazi kwa kumalizia ujenzi wa nyumba yake kwa kuiwekea marumaru ‘tiles’ pamoja na madirisha ya vioo,” kilisema chanzo hicho cha habari.

Ishu ya Kahata “Uongozi wa Simba upo katika hatua za mwisho kwa ajili ya kumalizana naye na umepanga kumsainisha mkataba mapema kabla ya kuanza majukumu ya kuitumikia timu yake ya taifa ya Kenya kwenye

Haruna Shamte

Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) baadaye mwezi ujao huko nchini Misri,” kilisema chanzo. Alipotafutwa Kahata mwenyewe alisema: “Ishu hiyo bado haijakamilika, nipo nyumbani Kenya nikiwa na timu ya taifa, tunajiandaa na Afcon ambapo kesho (leo) Ijumaa tunasafiri kuelekea Ufaransa kuweka kambi.”

Simba wanamtaka Kahata kuchukua nafasi ya Mganda Emmanuel Okwi ambaye anatarajia kuondoka ndani ya kikosi hicho. Shamte Haruna Shamte wa

Lipuli FC yeye tayari ameshamalizana na klabu hiyo kwenye mazungumzo ambapo imebaki suala la kusaini mkataba tu. “Analetwa maalum kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Zana Coulibaly ambaye ana uwezekano wa kuachwa pamoja na Shomari Kapombe ambaye amekuwa na majeraha ya mara kwa mara,” kilisema chanzo.

Inaelezwa kuwa Kocha wa Simba, Patrick Aussems anahitaji kusajili beki wa kati, beki wa kushoto, kiungo mkabaji pamoja na mshambuliaji

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *