YANGA yapata pigo kwa kuondokewa na Mjumbe Kamati ya Utendaji

Klabu ya Yanga, wadau na familia ya michezo kwa ujumla nchini Tanzania imepata pigo kufuatia kifo cha mjumbe wa kamati ya klabu hiyo Felix Kibodya.

Kifo cha Kibodya kimetokea usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Taarifa hizo pia zimethibitishwa na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela.

Mwakalebela amesema Yanga imepata pigo kutokana na msiba huo kwani walikuwa wanategemea nguvu kubwa kutoka kwa marehemu juu ya taaluma yake ya sheria.

Mwakalebela ameongeza kuwa kwa sasa klabu yao inafuatilia msiba huo kwa karibu kujua utaratibu kamili na kwamba baada ya hapo watatoa taarifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *