MO afunguka usajili Simba

Mwekezaji wa klabu ya Simba Mohamed Dewji almaarufu Mo amesema kwa sasa wanajiapnga vyema kuhakikisha wanawabakisha wachezaji wao wote wa ndani na wale kutoka nje ya Tanzania ili kuendelea kubaki na nguvu yao licha ya asilimia kubwa ya wachezaji hao kuwindwa na vilabu vikubwa Afrika.

Dewji amesema hayo wakati wa Tuzo za ‘MO SIMBA AWARDS’ zilizofanyika usiku wa njana ambapo amesema asilimia sitini mpaka sabini ya wachezaji wa ndani mikataba yao imeisha huku asilimia wachezaji wa kigeni takribani asilimia 80 mikataba yao ikiwa imeisha.

“Tuna changamoto nyingi, ya kwanza kwamba wachezaji karibu sitini au sabini ya wachezaji wa ndani (Watanzania) mikataba yao inakwisha, kwa hiyo tumepata changamoto kubwa kutoka vilabu vikubwa kutokana na Simba kufanya vizuri kimataifa.

“Changamoto nyingine kubwa ni Tanzania kufuzu AFCON, kwa hivyo wachezaji wetu wanawindwa na vilabu vikubwa kama Zamalek, Saoura (JS), Al Ahly na kadhalika na shabaha ni kuwabakisha na la pili kwa upande wa wachezaji wa nje asilimia 80 mikataba yao inakwisha. Kwa hiyo tupo tayari kushindana na klabu kubwa Afrika kwenye transfer market (dirisha la usajili),”amesema MO.

Katika msimu huu wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba walivunja mwiko kwa mara ya kwanza kwa timu kutoka Tanzania kuingia hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
Dewji amesisitiza kuwa bado shabaha yao ni kuona siku moja Simba inatwaa taji hilo lenye thamani kubwa kuliko mataji yote kwa ngazi ya vilabu barani Afrika.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *