Kipindupindu Chaua Mmoja Dar,Wengine 32 Walazwa.


Hayo yamebainishwa leo Mei 29 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati wa ziara yake jijini Dar kuangalia hali ya ugonjwa wa kipindupindu na homa ya Dengue

Amesema “Tumepokea Wagonjwa 32 katika mkoa wa Dar, kambi ya Amana wapo 13, Temeke 18 na Mwananyamala mgonjwa mmoja, hii ni kutokana na hali halisi ya kutozingatia usafi.”

Kufuatia mlipuko wa ugonjwa huo, Waziri Ummy amezitaka Halmashauri zote za mkoa wa Dar es Salaam kutoa adhabu kali kwa wanaotiririsha maji machafu wakati wa mvua

Amefafanua “Mstahiki Meya kasema adhabu ni Tsh. 30,000 nimewataka waongeze iwe Tsh. 200,000. Tunataka mtu aone ni bora kuita gari la maji taka kwa Tsh. 150,000 kuliko kulipa hiyo faini.”

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar, Dkt. Yudas Ndungile amesema sehemu kubwa ya Wagonjwa waliopatikana wanatoka eneo la Mchikichini na mabondeni ambako magari ya taka hayapo ila mipango inafanywa kufikisha magari hayo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *