Diamond aweka wazi itakapofanyika video ya INAMA

Msanii wa muziki maarufu zaidi kwa sasa nchini Tanzania, Diamond Plutnumz tayari ameingia jikoni kuanza maandalizi ya kufanya video ya wimbo wake mpya INAMA ambao amemshirikisha Fally Ipupa.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, Diamond akiwa jijini Paris na Mose Iyobo ameposti video akicheza staili ya kibaiskeli ambayo ndiyo hasa inayoutambulisha wimbo huo na kuandika maneno ambyo yanaashiria kuanza maandalizi ya kufanya video hiyo.

β€œVENYE TUNAINGIA MJINI PARIS UFARANSA KULISHOOT HILI GOMA LA #INAMA NA MWANANGU @moseiyobo πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„….KAHAMA VIDEO TUNALIACHIA RASMI PALE UWANJANI KWENYE #OneManOnemic EID MOSI !!!! #INAMADF,” ameandika Diaond Plutnumz.

Ngoma ya Inama imekuwa maarufu sana nchini Tanzania na nje ya mipaka ya Tanzania kutokana na staili yake ya uchezaji ambayo aliitambulisha kwa mashabiki wake.

Ikiwa na siku ishirini na tatu (23) mpaka sasa, ngoma ya Inama imefanikiwa kutazamwa na takriban watu milioni 2.5, idadi ambayo ni kubwa vya kutosha.

Hii ni mara ya kwanza kabisa kwa Diamond Plutnumz kushirikiana kutoa ngoma na Fally Ipupa ambaye anasifika kwa staili mbalimbali za uchezaji.

Huu ni mwendelezo wa Diamond Plutnummz kufanya collabo na wasanii mbalimbali maarufu na wakubwa. Ameshafanya collabo na Ne-Yo, Rick Ross kutoka Marekani, P Square, Davido, Patoranking na wengine wengi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *