Upande wa utetezi wataka upelelezi kukamilika katika kesi ya Kisena

 

 

Upande wa utetezi katika kesi inayomkabili Mkurugenzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (UDART) Robert Kisena (46) na wenzake umeutaka upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo ili hatua nyingine ziweze kuendelea.

Wakili wa utetezi Zuri’el Kazungu ameyaeleza hayo leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizire wakati shauli hilo lilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Kazungu aliomba upande huo wa mashtaka waseme ni lini watakamilisha upelelezi wa shauri hilo ili hatua nyingine ziendelee.

Baada ya maelezo hayo, Wakili wa Serikali Wankyo Saimon alidai upelelezi bado unaendelea na kwa mazingira ya shauri hilo maeneo yanayofanyiwa upelelezi ni mengi na hawaweze kueleza wamefikia wapi kwani ni mwezi mmoja tu umepita tangu washtakiwa kufikishwa mahakaman.
Hakimu Rwizile aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 6, mwaka huu kwa kutajwa na washitakiwa wamerudishwa rumande.

Mbali na Kisena washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni mkewe Frolencia Membe, Kulwa Kisena(33), Charles Newe(47) na raia wa China, Cheni Shi (32).

Watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 19 ikiwemo la kusababisha hasara kwa UDART ya Sh. Bilion.2.41.

Katika mashtaka hayo yapo ya Kuongoza genge la uhalifu, kujenga kituo cha mafuta bila kibali, kuuza mafuta sehemu zisizoruhusiwa, Wizi wa mafuta na utakatishaji fedha wa Sh. Bilioni.1.2, kughushi na kusababisha hasara ya Bilioni.1.4.

Katika shtaka la pili linawakabili washitakiwa wanne ambao ni Kisena, Kulwa, Simon na Florencia ambalo ni kujenga kituo cha mafuta ya petroli bila kibali kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).

Inadaiwa Januari Mosi mwaka 2015 na Desemba 31 mwaka 2017 walijenga kituo hicho eneo la Jangwani bila kibali.

Katika shitaka la tatu washitakiwa hao inadaiwa kwa kipindi hicho wakiwa wakurugenzi walifanya biashara eneo ambalo halijarusiwa kujengwa.

Katika kosa la utakatishaji fedha linalomkabili Robert Kisena na Chen Shi, Wakili Mwenda alidai kuwa Aprili 8, 2016 katika benki ya NMB Kisena akiwa Mkurugenzi wa UDART alihamisha Sh.Milioni 594.92 kwenda kwenye akaunti nyingine ya Kampuni ya Longway Engineering Company wakati akijua fedha hizo ni za haramu zililotokana na makosa ya kughushi.

Pia kosa la kuisababishia UDART hasara linawakabili washitakiwa wote ambapo inadai kuwa kati ya Mei 25, 2015 na Desemba 2016 wakiwa Dar es Salaam waliisababishia hasara UDART ya Sh. Bilioni.2.41.

Katika kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu linamkabili Kisena na Shi ambapo wanadaiwa walilitenda June 9 mwaka 2016 katika tawi la NMB Ilala ambapo kwa nia hovu walijipatia Sh Milioni 603.25 kutoka UDART kwa kuonyesha kiwango hicho kimelipwa kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa Kituo cha UDART Kimara, Ferry (Kivukoni), Ubungo na Morocco.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *