Harmonize amuomba radhi baba yake. Aahidi kutomwangusha

Msanii kutoka kundi la Wasafi Harmonize amemuomba radhi baba yake mzazi kwa kuamua kujiingia kwenye tasnia ya muziki kinyume cha matakwa yake.

Amesema baba yake Abdulkahali ni mtu mwenye misingi imara ya dini na hivyo kitendo cha mtoto wake kujiingiza katika tasnia ya muziki ni kitendo ambacho kilimuumiza.

Ameongeza kuwa licha ya kuwa katika masuala ya muziki, baba yake amekuwa akimsihi sana kufuata misingi ya dini japokuwa anajua fika kwamba baba yake bado anaamini mwanaye yupo nje ya misingi halali ya dini.

Katika kuomba kwake radhi, Harmonize amesema kuna mambo mawili, moja ni yeye kuamua kufuata ndoto zake lakini la pili inawezekana pengine huu ndio upande ambao Mungu amemwelekezea.

Lakini hajsita kudhihirisha mapenzi yake ya dhati kwa kwa baba yake na kwamba anajivunia sana kuwa na baba kama yeye.

Baba yake Harmonize ni mwalimu wa Madrasa na anaamini panapo majaaliwa atamfanyia mpango wa kwenda kuhiji katika Mji wa Makka na kuongeza kuwa baba yake amemlea vizuri sana katika misingi imara ya dini.

Amemshukuru baba yake kukubali kushiriki katika moja ya sehemu za video ya wimbo wake mpya wa Never Give Up

Kwa sasa Harmonize ni moja ya wasanii wanapendwa sana hapa nchini Tanzania kutokana na umahiri wake mkubwa wa kuimba unaochagizwa na sauti yenye kuvutia.

Soma ujumbe wake hapa chini…..

 

View this post on Instagram

 

Huyu ni Baba yangu mzazi mzee (Abdukahali) kifupi nimetoka katika familia ya Dini sana….!!! Shughuli zake ndio kama mnavoziona hapo anafundisha Madrasa nami ilinisaidia kunijenga kiimani na kuwa na hofu ya Mungu kiukweli hakupendezewa kabisa baada ya kusikia Mtoto wake kipenzi nimejiingiza katika Mambo ya sana…!!! Nichukue fursa hii kumuomba radhi baba yangu niseme pengine ni shida ama ndicho Mungu alichoniandikia kukifanya Kama mzazi najua uliumia sana kuona Mtoto naenda njia sio sahihi Lakini uliniombea na ukaridhia kwa Moyo mkunjufu niendele kufanya ila nisimsahau Mungu alietuumba Sote….!!!! Love you Dady mpaka ukakubali kuwa katika Video yangu hakika unanipenda na kuniombea heri mwanao 🙏🙏🙏 Najivunia kuwa na Baba kama wewe mzee #Abdukahali

A post shared by KONDEBOY (@harmonize_tz) on

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *