Uchaguzi wa mwaka wa 2022 ukiwadia, vyama vingi vimeripotiwa kuundwa kwa ajali ya uchaguzi mkuu.
Msajili wa vyama humu nchini amesema kuwa huenda kukawa na vyama zaidi kwenye historia ya vyama nchini.
Kwenye ripoti hiyo, vyama 30 vimesajiliwa pindi tu uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2017 ulipomalizika.
Kaimu msajili wa vyama vya kisiasa Anne Nderitu alisema tayari majina 32 ya wanasiasa maarufu wamefuzu kusajiliwa kumiliki vyama vipya.
Hata hivyo, haijabainika ni nyadhifa gani wanasiasa hao watawania ifikapo 2022.
Rais Uhuru Kenyatta hapo awali aliwaonya wanasiasa kutojihusisha na kampeni za mapema na kufanya kazi walioahidi wakenya.
Huenda wanasiasa walioshindwa mwaka wa 2017 wakajiunga na kinyanganyiro cha 2022 na vyama vipya.