Aliyekuwa mshirika wa Raila awakumbusha Wajaluo utabiri mchungu kuhusu Odinga uliokuja kutimia

Related image

Je, jamii ya Waluo imekuwa na uaminifu mkubwa kwa kiongozi wa ODM Raila Odinga hadi ikasahu kupigania ustawi wake?

Hili limekuwa hoja kubwa sana ambalo wakenya na wanasiasa wameliweka kipau mbele wakati huu jina Odinga inapokwaza vichwa vya waluo.

Hakuna pingamizi hata kidogo kwamba wajaluo ni waaminifu kwa Baba na mtu yeyote anayetafoutiana na yeye anaonekana kuwa adui wa jamii ya wajaluo. Haya yakijiri, itabainika wazi kuwa viongozi wengi wa Nyanza wamekuwa wakifuatilia baba na kusahau kukimu majukumu ya wakaazi waliowachagua.

Related image

Hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kuwa kuna baadhi ya viongozi kutoka jamii ya Luo ambao wameona mwangaza na kujiondoa kwa huo mkondo wa Raila ambao umeangamiza uchumi ya wajaluo.

Uchaguzi mdogo uliopita wa Ugenya ni dhahiri shahiri kuwa wajaluo wanakwepa mkondo wa Odinga.

Kuna visa vingi kwenye uchaguzi mkuu wa 2017 ambapo wabunge na wanachama wa county (MCA) walishinda bila kutumia chama cha Raila ODM.

Mashaka bado yamebaki kama jina la Raila litakuwepo kwenye debe mnamo mwaka wa 2022 au La ikikumbukwa kwamba aliyekuwa mbunge wa Ndiwa, Agostinho Neto alichukuwa muda wake wa Pasaka kuwakumbusha jamii ya wajaluo mbona ilikuwa na itakuwa ngumu kwa Raila kuwa rais.

Kulingana na Neto, alitabiri mwaka wa 2013 kuwa itakuwa ngumu kwa Raila kumenyana na kushinda Uhuruto kwa 2017, kitu ambacho kilikuja kutimia.

Image result for neto ndiwa

“Mwaka wa 2013 pale Bondo kwa tamasha ya ujio wa mheshimiwa Ochanda, nilikuwa mbunge kipindi hicho na niliwaambia wabunge wa jamii ya waluo kwamba Raila hatoweza kushinda Uhuruto kwa 2017. Hii haikuwa kwa sababu Raila hajulikani lakini kwa sababu kulikuwa na haja ya kuupanga mundo ili kupigana na Uhuruto. Wajaluo kwa njia yao wakanitusi na kunikashifu kwa kuwahurumia Jubilee lakini 2017 ulipita na alishindwa” asema Neto.

Neto amewaambia wajaluo kuwa njia mwafaka ya kuwa na rais mjaluo ni kushirikiana na makabila mengine haswa ya wakalenjin.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *