Wafuasi wa Zari washawishika kwamba wamefumbua uso wa ‘King Bae’

Related image

Mwanamtindo maarufu Zari the Boss lady amehakikisha kwa mda mrefu kwamba ameficha sura ya aneyedhaniwa kuwa mpenzi wake.

Baada ya kumwacha mume wake msanii wa Bongo Diamond Platinumz, Zari hajatulia kwenye mapenzi na kwa mda sasa amekuwa akizitia picha kwenye mtandaoni akiwa na ‘King Bae’.

Kwenye pilkapilka zetu za kupekua kwa Instagram, tulipata kujua baadhi ya wafuasi wake ambao walishawishika kwamba wamepata kumjua ‘King Bae’.

Image result for zari and king bae

Cha kushangaza ni kuwa, huyu anayedhaniwa kuwa mpenzi wake Zari ana mwonekano kamili na mdomo kama ule wa mpenzi maarufu na fiche wa Zari.

Kwa hiyo picha, Zari na huyu bwana msiri waliketi pamoja kwa ukaribiano mkubwa huku ameweka kichwa chake kwenye bega wa mtanashati huyu.

Vile vile, Zari alitia mkono moja kwa bega na nyingine kwa paja ya mtanashati kuashiria uhusiano wao wa karibu.

Hata hivyo, duru za kuaminika zinasema kuwa Zari atafanya harusi ya kufana hivi karibuni, lakini je? Sisi wakwe wa mitandaoni tutaalikwa?

Zari hapo awali alisisitiza kuwa iwapo atafanya harusi, hataiweka wazi na jamaa na marafiki tu ndio watahudhuria.

Hii ilitokana na shinikizo alizokumbana akiweka mambo yake ya familia na mapenzi kwenye wazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *