Jinsi kukamatwa kwa Muhammad Swazuri kumefichua uozo wa NLC

Related image

Maafisa wakuu wa ardhi walikamatwa hapo jana kwa tuhuma za kubadilisha bei ya ardhi isipofaa na pia kupokea hongo.

Aliyekuwa mkuu wa tume ya ardhi (NLC) Muhammad Swazuri, na maafisa wa ardhi pamoja na jamaa zao walizuiliwa kwa kushukiwa kujihusisha na malipo ya shillingi milioni 109 ya ardhi ambayo dhamana yake ni millioni 34.

Tume ya kukabiliana na ufisadi EACC iliwakilisha kesi kortini ambayo inaonyesha kwa ufasaha jinsi pesa ziliporwa.

Image result for muhammad swazuri

“Hii ni baadhi tu ya ununuzi isivyofaa kwa mashamba na miradi ya serikali iliyofanywa na NLC ikiwemo reli ya SGR,” alisema mchunguzi Catherine Ngari wa EACC.

Mkurugenzi wa mashtaka wa umma Noordin Haji alisema kuwa walithatmini thamani ya ardhi hiyo ambayo ilikuwa shillingi milioni 34.5 mwaka wa 2015. Lakini baada ya kampuni kukataa toleo hilo, Dtr. Swazuri akaamrisha uthatmini wa thamani upya.

Baada ya kufanya thatmin kwa mara ya pili, KeNHA ambayo ina mamlaka ya barabara kuu Kenya iliondoa shillingi milioni 109.7 kwa NLC. Tume ililipa milioni 55.2 kwa wakurgenzi wa Tornado Carriers-Asia Akhtar Nazir Ahmed na Tarah Begun Khan.

Image result for dpp haji
Noordin Haji

“Pesa zilizobaki zilipewa CW Chege Advocates ambaye aliwagawanyia maafisa wa NLC kama hongo,” ilisema EACC.

Pesa hizo zilisambazwa kupitia jamaa za maafisa wa NLC na biashara kwa nia ya kuficha siri za zile pesa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *