Sad!Nandy mourns the loss of her best friend

The ‘Ninogeshe’ hit maker, Nandy is yet to come into terms with the death of Clouds Media Group boss, Ruge Mutahaba. She has taken to social media to share an emotional letter to him. She wrote;

Kila mtu ana mtu ambaye ameumbwa na MUNGU kwa ajili yake. Na jinsi yakukutana na uyo mtu inaweza ikawa ni ndefu ikawa na matuta mara nyingine inaweza ikakuchosha lakini mwisho wa siku kila kitu kinakuja kuwa sawa.. Wanaweza kutokea watu wachache ambao watakuelewa na pia kuelewa ndoto zako hata kama unazifanya mwenyewe..

Watakuwa hapo kukupa mrejesho chanya na watakubeba kwenye safari yako kwa moyo wote… Watanzania wanakupenda Umegusa maisha ya watu kwa namna tofauti tofauti Ulizaliwa kuwa kiongozi Ulikuwa na moyo wakutoa.. Ruge ulikuwa rafiki yangu wa karibu sana, ulikuwa kila kitu kwangu Ruge ulielewa ndoto yangu Ruge ulinipa moyo wa kupambana hata kama nilikua nataka ku give up Ruge uliona ndoto yangu na hukuwa na wasiwasi nayo….

Ulivo pumzika naweza kukuhakikishia…Nitakufanya ujivunie…Nitaendelea kuzi enzi na kuziishi hekima zako. Na nitafanya juhudi kufikia malengo tuliyo panga pamoja.. Nakupenda sana na nitaendelea kukupenda hata kama haupo nasi. YOUR THE BEST THING THAT EVER HAPPEN TO ME
ROHO YANGU.. R.I.P”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *